Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema Makosa mbalimbali ambayo yanafanywa na wanaoendesha vyombo vya moto barabarani yamesababisha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupata zaidi ya Sh.Bilioni 2.74.
Mambosasa aliyasema hayo jana ambapo alifafanua kuwa jeshi hilo linaendelea na operesheni ya kuwasaka madereva wa magari na watumiaji wa vyombo vya moto ambao hawazingatii sheria ya usalama barabarani.
Alisema katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata magari madogo,maroli, pikipiki na daladala ambapo wahusika wametozwa faini ambapo zaidi ya Sh.Bilioni 2.74 zimepatikana.
Kamanda Mambosasa amewawataka watu ambao wametozwa faini za barabani kulipa kwa wakati kwani kuna tabia ya kulimbikiza deni na wataendelea kuwasaka wadaiwa wote na iwapo watashindwa gari litachukuliwa na kuwekwa Polisi.
Social Plugin