Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu mkoa wa Kagera kusimamia zao la kahawa na kuwachukulia hatua kali wanaojihusisha na magendo ya kahawa ikiwemo baadhi ya askari wa jeshi la Polisi.
Ikiwa ni siku ya pili tangu waziri mkuu aanze ziara yake ya kikazi mkoani Kagera,ametembelea chama cha msingi cha Nkwenda na kuongea na wananchi kwenye mkutano wa adhara katika viwanja vya chama hicho na kumtaka mkuu wa mkoa wa Kagera brigedia jenerali Marco Gaguti na Kamanda wa polisi wa mkoa huu Augustine Ollomi kudhibiti magendo ya kahawa ambayo yameshamili wilayani Kyerwa.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa ataendelea na ziara yake ya kikazi hapo kesho katika wilaya ya Biharamulo na Muleba baada ya kumaliza wilaya ya Kyerwa na Karagwe
Na Angela Sebastian -Malunde1 blog
Na Angela Sebastian -Malunde1 blog
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa
Social Plugin