Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, LazaroMambosasa amezungumza leo mchana kuhusiana na tukio la kutekwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mo Dewji ambapo amesema hadi mchana huu taarifa rasmi ni kwamba Mo bado hajapatikana na watekaji bado hawajakamatwa.
Mambosasa amewataka wananchi kuzipuuza taarifa zinazosambaa mitaani kwamba Mo kapatika akiwa Coco beach kwa kuwa ni za uongo na wala hazijatolewa na ofisi yake.
Amesema jeshi la polisi linaendelea na Opareshen kali kwa kushirikisha mikoa mitatu kuhakikisha Mo Dewji anapatikana na watekaji wanatiwa Mbaroni
Social Plugin