Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMUUA BABA YAKE KWA KUMKATA SHOKA KISA KAMNYIMA MAHARI


Jeshi la Polisi mashariki mwa mji wa Eldoret, kaunti ya Uasin-Gishu magharibi mwa Kenya imemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 28, Andrew Kimutai, akituhumiwa kumuua baba yake, Joseph Marindany.

Akithibitisha tukio hilo OCPD wa Eldoret Mashariki Bw Richard Omanga, amesema kuwa Andrew anatuhumiwa kumuua baba yake kwa kumkata kichwa kwa kutumia shoka, baada ya kukataa kumpa kondoo wa familia ili alipe mahari kukomboa mtoto wake wa kiume aliyempata nje ya ndoa.

“Marehemu alikataa kumpa mwanawe kondoo kwa sababu hakujua alikuwa amezaa mtoto nje ya ndoa kama alivyodai. Mshukiwa alikasirishwa na msimamo wa baba yake ndipo alimvamia baba yake akiwa chumbani mwendo wa saa moja, akamkatakata kwa shoka,” alisema OCPD Omanga.

Mtuhumiwa huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Naiberi akisubiri kufunguliwa mashtaka baada ya uchunguzi kukamilika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com