Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MANYIKA JR ALAMBA DILI KENYA


Manyika Jr akisaini mkataba.

Aliyekuwa mlinda mlango wa timu ya Singida United Peter Manyika Jr, amejiunga na klabu ya KCB inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.

Akiongea na www.eatv.tv baba mzazi wa Manyika Jr, Peter Manyika amesema kijana wake amesaini mkataba huo Oktoba 25, 2018.

''Ni kweli kijana amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuichezea klabu ya KCB hivyo kwasasa ni mchezaji wa timu hiyo'', amesema.

Manyika amejiunga na klabu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya kuondoka Singida United kutokana na kushindwa kulipwa stahiki zake ikiwemo malipo ya usajili na mishahara.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com