Msichana mmoja raia wa Uingereza aliyejulikana kwa jina la Gemma Evans amemgonga mtu mmoja aliyekuwa akiendesha baiskeli na kufariki papo hapo wakati alipokuwa akituma ujumbe wa katuni katika mitandao ya Whatsapp na Facebook huku akiendesha gari.
Gemma (23) alikuwa akitumia simu yake kutuma ujumbe wa katuni za utani katika mitandao hiyo huku akiendesha gari asubuhi alipokuwa akitoka kazini baada ya kufanya kazi usiku mzima.
Yeye mwenyewe ameeleza kuwa pindi inatokea ajali hiyo simu yake ilikuwa katika mkoba wake na hakuitumia katika safari nzima hadi tukio hilo linatokea.
Polisi imemkatata msichana huyo na katika uchunguzi uliofanyika kwa kutumia simu yake na kwa msaada wa kamera za barabarani, imemuonesha dereva huyo akichepuka upande wa pili ambao ndio tukio hilo lilikotokea.
Wakati inasikilizwa kesi hiyo katika mahakama ya Merthyr Tydfil, jaji alisikika akisema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi wa maafisa wa polisi, imeonesha msichana huyo alikuwa akiwasiliana kwa ujumbe wa katuni na rafiki yake katika mitandao kabla ya kuacha njia yake na kumgonga mwendesha baiskeli huyo aliyejulikana kwa jina la Diane Prince mwenye umri wa miaka 58.
Hakimu ameeleza zaidi kuwa taarifa hiyo ya maafisa wa polisi imeelenda mbali zaidi kwa kuelezea maudhui ya ujumbe huo uliosababisha ajali, ikisema kuwa msichana huyo alikuwa akipanga mtoko wa usiku na rafiki yake huyo ambaye alikuwa akiwasiliana naye
Social Plugin