Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : DC MBONEKO AZINDUA KAMPENI YA ELIMU YA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI...MAASKOFU WASEMA WAMECHOKA KUZIKA



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste mkoa wa Shinyanga pamoja na kuzindua kampeni ya kutolewa elimu ya sheria hizo kwa wananchi.


Mboneko amefunga mafunzo hayo,leo Oktoba 20, 2018 kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Shycom mjini Shinyanga, akimwakilisha mkuu wa mkoa huo Zainab Telack.

Hafla hiyo ya ufungaji mafunzo imehudhuriwa na wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa usalama barabarani.

Mboneko amesema elimu hiyo ya Sheria za usalama barabarani iliyotolewa kwa viongozi hao wa dini, ni jambo la maana kwa sababu wao wakielimika watakuwa mabalozi wazuri wa kutoa elimu kwa waumini wao, na hatimaye kuweza kumaliza ama kupunguza kabisa tatizo za ajali, ambalo limekuwa likigharimu maisha ya watu.

“Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na chuo cha mafunzo ya Sheria za usalama barabarani New Vision, kwa kutoa mafunzo haya kwa viongozi hawa wa kidini, ambao watakwenda kutoa elimu zaidi kwa waumini wao, na kuepukana na ajali zisizo za lazima,”amesema Mboneko.

“Kwa takwimu za nyuma mkoa wa Shinyanga ndani ya mwezi mmoja kulikuwa kunatokea ajali 17, lakini kwa sasa tangu elimu hii ya Sheria za usalama barabarani ianze kutolewa kikamilifu, sasa hivi ndani ya mwezi huo zinatokea ajali tano, hali ambayo tunaelekea kuzuri kwenye kuondokana kabisa na ajali,”ameongeza.

Pia ameliagiza Jeshi la Polisi kuzuia mikokoteni kuingia katikati ya Mji na kuikamata ile ambayo haina Viakisi mwanga, pamoja na kuendelea kutoa elimu ya sheria za usalama barabarani kwa madereva wa vyombo vya moto, zikiwamo na daladala za baiskeli.

Naye mwenyekiti wa Makanisa hayo ya Kipentekoste Mchungaji Elias Madoshi,amesema viongozi hao wa kidini watashirikiana na Jeshi la Polisi kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wananchi kupitia madhabahu yao, kwa sababu wamechoka kuwa wanazika watu wanaofariki na ajali.

“Tumechoka maaskofu kuwa tunazika watu wanaofariki kwa ajali, ambapo tumekuwa tukisema bwana ametoa na bwana ametwaa, vifo vya ajali siyo bwana ametwaa ni kujitakia, hivyo nawaomba wananchi na madereva wa vyombo vya moto tuzitii sheria za usalama barabarani tuepukane na ajali za kizembe,”amesema Madoshi.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi, Askofu Mungo Makundi kutoka Kanisa la TAG Jimbo la Shinyanga  amesema baada ya kuona viongozi hao wa kidini wanaendesha vyombo vya moto bila ya kuwa na mafunzo ya Sheria za usalama barabarani huku wakiwa na Leseni, ndipo wakaomba wapatiwe mafunzo hayo.

Amesema mafunzo hayo yalianza Septemba 27 mwaka huu na kuhitimishwa Oktoba 11, ambapo jumla ya Maaskofu na wachungaji 173 wa makanisa hayo ya Kipentekoste wamehitimu.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifunga rasmi mafunzo ya Sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 Blog

Kamanda mkuu wa kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Shinyanga Richard Abwao akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani humo Simon Haule ambapo amepongeza mafunzo hayo kwa viongozi hao wa dini ambayo yatasaidia kupungaza ajali.

Askofu Mungo Makundi kutoka Kanisa la TAG Jimbo la Shinyanga,akisoma risala ya viongozi wao wa kidini kwenye hafla hiyo ya kufunga mafunzo pamoja na uzinduzi wa kampeni ya sheria za usalama barabarani kwa wananchi.

Mwenyekiti wa makanisa ya Kipentekoste mkoani Shinyanga Mchungaji Elias Madoshi, akizungumza kwenye hafla hiyo na kudai kuwa Maaskofu na wachungaji wamechoka kuzika watu wanaofariki na ajali zitokanazo na uzembe.

Balozi wa usalama barabarani Kanda ya Ziwa Abel Ntaho akizungumza kwenye hafla hiyo na kuomba wananchi kuacha tabia ya kuharibu miundombinu ya usalama barabarani.

Maaskofu na wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste mjini Shinyanga wakiwa kwenye hafla ya kufunga mafunzo yao ya kuhitimu Sheria za usalama barabarani.

Wadau wa usalama barabarani wakiwa kwenye hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo ya Sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste mjini Shinyanga.

Maaskofu wa madhehebu mbalimbali wakiwa meza kuu, ambao wamealikwa kushuhudia zoezi hilo la ufungaji wa mafunzo ya Sheria za usalama barabarani pamoja na uzinduzi wa kampeni ya elimu hiyo kwa wananchi.

Wananchi wakiwa kwenye hafla hiyo.

Maaskofu na wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste mjini Shinyanga wakiwa kwenye hafla yao ya ufungaji wa mafunzo ya Sheria za usalama barabarani.

Wananchi wakiwa eneo la tukio.

Wanafunzi wakiwa eneo la tukio.

Wananchi wakiwa eneo la tukio.

Wananchi wakiwa eneo la tukio.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya sheria za usalama barabarani Askofu Jakobo Madaha.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya sheria za usalama barabarani mama askofu Agnes Ndaki.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi tuzo ya kufanya vizuri kusimamia Sheria za usalama barabarani pamoja na kupunguza tatizo la ajali mkoani Shinyanga (RTO) Anthony Gwandu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi tuzo ya kufanya vizuri kusimamia Sheria za usalama barabarani pamoja na kupunguza tatizo la ajali wilaya ya Shinyanga (DTO),Emmanuel Pallangyo.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga (DTO), Emmanuel Pallangyo akimpigia Saluti boss wake mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Shinyanga (RTO) Athony Gwandu mara baada ya kumaliza kupewa tuzo ya kusimamia sheria vizuri na kupunguza ajali.

mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi Tuzo Pc Fatima All kwa kusimamia vizuri sheria za usalama barabarani.

Tuzo zikiendelea kutolewa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi tuzo ya kutoa elimu ya usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji mratibu wa mafunzo ya Sheria hizo kutoka chuo cha New Vision cha jijini Dar es salaam Deogratius Kidana.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi tuzo ya kutoa elimu ya usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji mratibu wa mafunzo ya Sheria hizo kutoka chuo cha New Vision cha jijini Dar es salaam Seif Ahmad Luyangi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi tuzo Barozi wa usalama barabarani Kanda ya Ziwa Abel Ntaho.

Awali mwenyekiti wa umoja wa mabaraza ya makanisa ya Kiinjili Tanzania David Yegela akitambulisha wageni.

Wana kwaya wa Kanisa la AICT Kambarage wakitoa burudani kwa kuimba nyimbo za kutii sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali.

Wana kwaya wa Kanisa la AICT Shinyanga wakitoa burudani kwa kuimba nyimbo za kutii sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali.

Wana kwaya wa Kanisa la FPTC Kanani mjini Shinyanga wakitoa burudani kwa kuimba nyimbo za kutii sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali.

Wanafunzi wa shule ya Little Treasures nao wakitoa burudani ya kuimba nyimbo za kumaliza ajali.

Wakuu wa usalama barabarani wilaya ya Shinyanga ,Kishapu na Kahama wakiongoza maandamano kuelekea kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya Sheria za usalama barabarani kwa maaskofu,wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste pamoja na kuzindua kampeni ya sheria hizo kwa wananchi.

Wanafunzi wakiwa wamebeba mabango.

wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kutii sheria za usalama barabarani.

Maaskari wa usalama barabarani wakiwa kwenye maandamano.

Bodaboda nao wakiwa kwenye maandamano.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (katikati) akipokea mandamano, Kushoto ni RTO Athony Gwandu, na kulia ni mwenyekiti wa makanisa ya Kipentekoste Elias Madoshi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiingia na msafara wake kwenye halfa ya kufunga mafunzo ya Sheria za usalama barabarani pamoja na kuzindua kampeni ya Sheria hizo.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 Blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com