Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MNEC MTEWELE ACHANGIA MIFUKO 50 YA SARUJI KWA AJILI YA UKARABATI WA SHULE YA MSINGI NJIA PANDA


Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa (MNEC) Theresia Mtewele akimkabidhi cheti cha kuhitimu darasa la saba mwanafunzi wa shule ya msingi Njia Panda


Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa (MNEC) Theresia Mtewele akicheza kwa furaha na wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya msingi Njia Panda.
Mjumkbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa (MNEC) Theresia Mtewele akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wahitimu wa darasa la saba wa shule ya msingi Njia panda.

NA FREDYE MGUNDA,IRINGA.

MJUMBE wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa (MNEC) Theresia Mtewele amechangia mifuko hamsini ya saruji katika shule ya msingi Njia panda ambayo inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa kumi na nane pamoja na matundu thelathini na saba ya vyoo na kusababisha kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza wakati wa mahafali ya shule hiyo MNEC mtewele alisema kuwa hali ya miundombinu ya shule hiyo sio rafiki kwa wnafunzi kupata elimu bora kama ambavyo serikali ya awamu ya tano inakusudia.

"Naiomba Serikali na wahisani mbalimbali kuisaidia shule ya msingi hii kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo ili kuwawekea mazingira bora ya kusoma wanafunzi ya kufanya vizuri kwenye mitihani yao",alisema Mtewele

Mtewele alisema kuwa kwa mazingira ambayo ameyaona ya miundombinu ya shule hiyo inahitajika nguvu ya ziada kuhakikisha wanatatua changamoto hizo ambazo zimekuwa kikwazo cha kufanya vizuri kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo

"Leo sijalidhishwa na hali hii japo nimekuja kumuwakilisha mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Salim Asas nitaenda kumueleza ukweli jinsi ambavyo shule hii inahitaji msaada mkubwa na wa haraka kwa kuokoa elimu ya wanafunzi Hawa" alisema Mtewele.

Aidh MNEC Mtewele aliwaasa wahitimu na wanafunzi wanaoendelea wasikubali kurubuniwa na watu wasiowafahamu kw kuwa watawakatisha ndoto zao za baadaye zaidi wajikite katika masomo na kujiepusha na magonjwa ambukizi.

Dunia ya sasa inaharibiwa sana na watu ambai wanatumia vibaya mitandao ya kijamii hivyo ni lazima mjue jamii ambayo mnaishi nayo inamalengo gani na je inafaida katika maisha yako ya baadae ndio upate muelekeo na maamuzi sahihi kwa faida yako alisisitiza MNEC Mtewele.

Mtewele ameuahidi uongozi wa shule kufuatilia utekelezaji wa ahadi kwa wabunge wote wa Mkoa wa Iringa ambao walitoa ahadi zao katika shule hiyo miaka ya nyuma na ahadi hizo hazikutekelezwa mpaka sasa.

Katika risala iliyosomwa na Mwalimu mkuu wa Federika Mahembepo shule hiyo alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa zaidi ya madarasa 18 na matundu ya vyoo 37 ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo.

Lakini mealimu mkuu wa shule hiyo amewapongeza walimu na wazazi wa shule hiyo kwa kutambua kazi ngumu na nzito wanayofanya kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu inayosatahili kama ambavyo wanafunzi wengine wanapata Elimu bora na kuwaomba wazazi waendelee kuiunga mkono serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa sababu imedhamilia kushughulika na shida za watu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com