Mfanyabishara Mo Dewji amerudi mtandaoni kwa mara kwanza toka atekwe na watu wasiojulikana na baadae kuachiwa na watekaji hao akiwa salama.
Bilionea huyo alitekwa alfajiri ya Oktoba 11 na kumuachia huru usiku wa manane wa Oktoba 20 baada ya msako mkali wa jeshi la polisi.
Jumatatu hii Mo ambaye pia ni mwekezaji wa klabu ya Simba, ametweet kwa mara ya kwanza kuwashukuru watanzania ambao walikuwa wanamuombea katika kipindi chote kigumu alichopitia.
“Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu. Pamoja na kupitia kipindi kigumu lakini daima amesimama upande wangu. Marafiki zangu, napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri. Mungu awazidishie kwa wema wenu. Baraka za Mungu ziwe nanyi leo na daima,” alitweet jana jioni
IGP Simon Sirro ameapa kuwatia nguvuni wakiwa wapo hai ama wamefariki, watu ambao wamtemka mfanyabishara huyo lakini leo ni siku ya tatu toka wamuachie bado hawajapatikana.
Social Plugin