Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Bilionea/Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo’ aliyetekwa na watu wasiojulikana Oktoba 11,2018 amepatikana akiwa hai.
Mo Dewji amepatikana alfajiri ya leo Jumamosi Oktoba 20, 2018.
Baba mzazi wa Mo Dewji, Gullam Dewji amesema,"Ni kweli Mo amepatikana, yupo hapa nyumbani."
Mo Dewji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya METL, Mohammed Dewji (MoDewji) amepatikana na kurudi nyumbani kwake salama, leo saa 9 na dakika 15 Alfajiri.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya METL, Mohammed Dewji (MoDewji)
Baba Mzazi wa Mohamed Dewji , Mzee Gulam Hussein amethibitisha mwanaye kupatikana na kurudi nyumbani salama.
Pia 'personal Assistant ' (PA) wa Mohammed Dewji Barbara Gonzale ameithibitisha kuwa amepatikana na kuzungumza maneno yafuatayo;
“Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama.” — Mohammed Dewji
Wakati huo huo Waziri January Makamba amesema amefika nyumbani Mo Dewji na kumuona kisha akaandika;
"Nimemuona na kuongea kwa kirefu na Mohammed Dewji. Ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni. Mnamo saa nane usiku, watekaji waliamua kumtupa kwenye maeneo ya viwanja vya Gymkana. Naamini Polisi watatoa taarifa za ziada kuhusu kilichojiri.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, amesema,
"Mo Dewji amepatikana akiwa mzima wa afya, baada ya kumhoji anasema alivyotekwa pale Collesium gari ilitembea kwa speed kama dakika 15 na kuwekwa mahali kama kwenye chumba".
Social Plugin