Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mo Dewji amewahakikishia mashabiki wa klabu ya Simba kuwa Uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo utakamilika kama alivyopanga ili kutimiza ahadi yake.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mo Dewji amesema anafanya hivyo kumalizia ujenzi wa uwanja huo ili utumike hata kama yeye asipokuwepo duniani.
“Tumefika hatua nzuri ya maendeleo ya uwanja wetu wa mazoezi wa #SIMBA. Nafurahi kuona maono yangu yanakamilika ili hata siku nisipokuwepo duniani, uwanja uendelee kutumika kwa mazoezi Insha’Allah.” ameandika MO.
Social Plugin