Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wakili Revocatus Kuuli amejiuzulu wadhifa huo.
Kuuli amefikia hatua hiyo kwa kumuandikia barua Rais wa TFF, Walace Karia iliyoeleza kujiuzulu nafasi ya Uenyenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF.
Kuuli ameeleza sababu ya kufanya maamuzi hayo ni kutokana na kuingiliwa majukumu yake ya kazi na katibu mkuu wa TFF Wilfred Kidao.
Hivi karibuni Kuuli alitangaza kuupiga STOP mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba baada ya kubainika ulikuwa na mapungufu kadhaa, na baadaye Kaimu Katibu Mkuu, Wilfred Kidao akamjia juu.
Kidao alikuja na kumtaka kuandika barua ya maelezo ikimtaka aeleze maamuzi hayo ameyatoa wapi huku akipewa siku tatu pekee awasilishe majibu.
Baada ya kupewa amri hiyo Kuuli alimjia juu pia Kidao na kueleza kuwa hawezi kuingiliwa katika majukumu yake na mpaka imepelekea atangaze maamuzi ya kuachia ngazi.
Social Plugin