Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : SHIRIKA LA OPE LAENDESHA MAFUNZO KWA WADAU WA ELIMU KUHUSU UTAFITI WA KKK




Shirika lisilo la kiserikali OPE la mkoani Shinyanga linalofanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwamo kukuza elimu, limeendesha mafunzo juu ya kufanya utafiti wa kubaini uwezo wa wanafunzi wenye kuanzia umri wa miaka 6 hadi 16, kama wanajua kusoma,kuandika na kuhesabu (KKK Tatu).

Semina hiyo iliyoanza leo,inafanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa Katemi Hotel ,mjini Shinyanga kwa kukutanisha wadau wa elimu kutoka asasi mbalimbali za kiraia kutoka mikoa ya Geita, Simiyu,Kigoma,Singida na Shinyanga ambao watafanya utafiti huo, na taarifa yake kuiwasilisha serikali.

Akizungumza leo Oktoba 17,2018,  Mkurugenzi wa Shirika hilo la OPE William Shayo amesema mafunzo hayo wanayaendesha kwa kushirikiana na Shirika la TWAWEZA, kwa lengo la kujua tatizo la wanafunzi kutokujua KKK Tatu, na kulitafutia ufumbuzi ilikukuza kiwango cha elimu hapa nchini.

Amesema utafiti huo utakuwa ukifanyika kwenye makazi ya watu pamoja na shuleni,kwa kushirikisha wanafunzi hao wenye umri kuanzia miaka 6 hadi 16 pamoja na walimu wao, ilibaini uwezo wao wa kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, pamoja na kubaini changamoto za wale ambao hawajui KKK Tatu na kuzitafutia ufumbuzi.

“Washiriki wa mafunzo haya mara watakapomaliza ndani ya siku hizi tatu, tayari wanaingia kazini kwenda kufanya utafiti huo wa kujua uwezo wa wanafunzi kusoma,kuandika na kuhesabu, na taarifa hizi tutaziwasilisha serikali na kwa wadau wa elimu, ilizipate kufanyiwa kazi na kuweza kumaliza kabisa tatizo la wanafunzi ambao hawajui KKK Tatu,”amesema Shayo.

Naye mgeni Rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo Katibu tawala la wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, akimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo Jasinta Mboneko, amepongeza semina hiyo kwa madai kuwa itaisaidia Serikali kubaini tatizo la baadhi ya wanafunzi kutokujua KKK Tatu, na kulitafutia ufumbuzi.

Aidha amewataka washiriki wa mafunzo hayo pale watakapokuwa kazini wafanye ufatifi wao kwa makini zaidi, ilikubaini kiini cha tatizo la wanafunzi kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu, na siyo kuweka mawazo yao binafsi jambo ambalo halitasaidia kumaliza changamoto hiyo wanafunzi kutokujua KKK Tatu.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Fatuma Abdala kutoka mkoani Geita ametoa wito kwa wazazi na walimu, pale watakapo kuwa wakifanya utafiti huo wawape ushirikiano ili kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mkurugenzi wa Shirika la OPE Mkoani Shinyanga William Shayo, akizungumza kwenye mafunzo hayo na kuelezea madhumuni ya kufanya utafiti huo wa kujua uwezo wa wanafunzi wenye kuanzia umri wa miaka 6 hadi 16 kama wanajua kusoma,kuandika na kuhesabu (KKK Tatu).Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniphance Chambi akizungumza kwenye mafunzo hayo, na kuwataka washiriki wayazingatie ili kuleta tija kwa Serikali kubaini kiini cha tatizo la wanafunzi kutokujua kusoma,kuandika na kuhesabu (KKK) na kuweza kulitafutia ufumbuzi,ilikukuza kiwango cha elimu hapa nchini.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Mafunzo yakiendelea.

Mmoja wa wawezeshaji kwenye mafunzo hayo George Maganga akiendelea na somo.

Washiriki wa Mafunzo wakisikiliza kwa makini.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com