Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KARDINALI PENGO : INJILI PEKEE HAITOSHI KUHUBIRI AMANI


Mwadhama, Polycarp Pengo

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo amesema injili peke yake haitoshi kuhubiri amani bali kuna taasisi nyingine ikiwemo serikali na dini nyingine ambazo zinapaswa kusimamia suala hilo.

Kardinali Pengo ametoa kauli hiyo leo Ofisini kwake St.Joseph, jijini Dar es salaam wakati akiongea na wanahabari ikiwa ni kuelekea sherehe ya miaka 150 ya usambazaji wa injili nchini ambayo ilianzia mjini Bagamoyo.

“Shughuli za kuinjilisha zinaendelea katika mfumo wa kibinadamu, kwanza injili haiko peke yake kwenye sehemu yetu ya Tanzania bara na maeneo mengine, kama wadau wa amani na maelewano, tuna sababu za kutokuwa na maelezo kwenye vitu vingine mnavyovisema kama chokochoko ”, amesema.

“Huwezi ukasema ni failure (kushindwa) ya uinjilishaji peke yake kwa sababu wadau wa amani ni pamoja na serikali watu wa dini na madhehebu mbalimbali, wote tunagombania amani, wote tunategemea watu kupiga hatua.”,ameongeza Kardinali Pengo.”

Aidha, Kardinali Pengo amesema mbali na changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii ni vyema watu wakatambua umuhimu wa kutunza misingi ya umoja na amani iliyopo ili kuweka kizazi kijacho katika mazingira bora ya upendo na mshikamano huku akionesha kusikitishwa na vitendo vya baadhi ya Makanisa kuwa na migogoro ambayo inapunguza imani ya waumini kwenye makanisa yao.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com