Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), akimkabidhi kadi ya matibabu Mwanamuziki Mkongwe, Mzee Makassy jijini Dar es Salaam leo wakati wa mkutano wa fursa kwa Wanaumoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO) ambapo pia alitoa kadi za matibabu za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa wanamuziki mbalimbali kupitia Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NNSF). Kutoka kushoto ni Rais TAMUFO, Dk.Donald Kisanga, na Mlezi wa TAMUFO , Mhandisi Juliana Pallangyo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), akimkabidhi kadi ya matibabu Mwanamuziki, Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kiki.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), akimkabidhi kadi, Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), akimkabidhi kadi, Mkurugenzi Mtendaji wa Bendi ya African Stars (Twanga Pepeta), Asha Baraka.
Wadau wa muziki wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mshereheshaji MC wa mkutano huo akiwa katika vazi la Kinaijeria.
Wadau wa mkutano.
Ofisa Mkuu Mwandamizi Kitengo cha Sekta Isiyo Rasmi kutoka NNSF, Abbas Cothema, akitoa mada.
Meza kuu.
Mwanamuziki Salim Mohamed Zahoro akizungumza.
Mzee Makassy akizungumza.
Mwanamuziki King Kiki, akizungumza.
Mlezi wa TAMUFO, Mhandisi Dk. Juliana Pallangyo, akiteta jambo na wadau wa muziki.
Wanamuziki wakiserebuka wakati wakimkaribisha Mhe.Ndugulile kuzungumza nao.
Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel, akizungumza.
Rais wa TAMUFO, Dk.Donald Kisanga, akizungumza.
Wadau wa muziki wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Dk. Ezekiel Kyogo akitoa mada kwenye mkutano huo.
Waimbaji wa Kwaya ya Sayuni wakiwa kwenye mkutano huo.
Maombi yakifanyika.
Mheshimiwa Ndugulile, akizungumza na wanamuziki hao.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, akimkabidhi kadi, Maria Joseph.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, akimkabidhi kadi, Hellen Makundi.
Kadi zikiendelea kutolewa.
Mhe.Ndugulile, akipiga picha na viongozi wa TAMUFO.
Mhe.Ndugulile, akimkabidhi kadi mwanamuziki wa Injili, Boniface Mwaitege.
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
WASANII wametakiwa kutumia sanaa yao kutoa elimu ili jamii iachane na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimeshamiri nchini.
Mwito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile Dar es Salaam leo wakati akizungumza katika mkutano wa fursa kwa Wanaumoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO) ambapo pia alitoa kadi za matibabu za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kupitia Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NNSF).
"Siku hizi kumekuwa na matukio mengi ya ukatili wa kijinsia ukihusisha masuala ya mapenzi na mambo mengine tuna waomba ninyi wasanii kupitia sanaa yenu tungeni nyimbo zitakazotoa elimu ya jamii kuachana na vitendo hivyo" alisema Ndugulile.
Alisema Serikali inatambua TAMUFO na ndio maana amefika kushiriki nao katika mkutano huo kutokana na mchango mkubwa wa wanamuziki katika taifa letu.
Alisema sanaa ni ajira na kuwa inachangia pato la taifa kutokana na kodi wanaliyolipa.
Aliongeza kuwa wajibu wa serikali ni kuhakikisha kila mtu anakuwa na afya bora wakiwemo wanamuziki na katika kutekeleza hilo inajenga vituo vya afya 67 katika kila wilaya na kuwa bajeti yake imepanda kutoka sh.bilioni 31 hadi kufikia sh.bilioni 270 kwa mwaka huu wa fedha wa 2017/2018 na kuwa mpango wa serikali ni kila mtanzania kuwa na kadi ya NHIF.
Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga alisema mkutano huo ni muhimu kwao kwa kuwa unawahamasisha wanamuziki kujiunga na mfuko huo wa bima ya afya wakiwa na lengo la kuwasaidia pale wanapoumwa waweze kutibiwa tofauti na ilivyo sasa .
Akitoa mada kwenye mkutano huo Ofisa Mkuu Mwandamizi Kitengo cha Sekta Isiyo Rasmi kutoka NNSF, Abbas Cothema alisema ni muhimu kwa wanamuziki kujiunga na mfuko huo ambao ni mkombozi kwao siku za usoni.
Alisema kupitia NSSF wameweza kuwaunganisha wanamziki kadhaa na NHIF ambapo walikuwa wakikabidhiwa kadi zao za matibabu.
Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Dk. Ezekiel Kyogo akitoa mada kwenye mkutano huo alisema ni muhimu kwa wanamuziki kuzijua sheria na kuwepo uzimamizi mzuri wa sheria hizo ili kulinda kazi za wasanii ili ikitokea mtu yeyote kuzikiuka akamatwe na sheria ichukue mkondo wake.
Social Plugin