SIKU moja baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo),
kuibua tuhuma za mauaji ya wananchi zaidi 100 katika Wilaya ya Uvinza
mkoani Kigoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno, amesema
taarifa hizo hazina ukweli.
Kamanda Ottieno alisema Zitto amezungumza upotoshaji na anatafuta umaarufu kupitia tukio hilo hivyo apuuzwe.
Kamanda Ottieno alisema ukweli uliopo ni kwamba askari wawili na
wananchi wawili ndiyo waliopoteza maisha katika mapigano ya jamii ya
wafugaji.
SIKU moja baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo),
kuibua tuhuma za mauaji ya wananchi zaidi 100 katika Wilaya ya Uvinza
mkoani Kigoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno, amesema
taarifa hizo hazina ukweli.
Kamanda Ottieno alisema ukweli uliopo ni kwamba askari wawili na
wananchi wawili ndiyo waliopoteza maisha katika mapigano ya jamii ya
wafugaji.
Juzi, Zitto aliwaambia waandishi wa habari kuwa mauaji hayo yalitokea
kwenye mapigano kati ya polisi na Wanyantuzu wilayani Uvinza, takribani
siku 11 zilizopita.
Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, alidai kuwa katika tukio
hilo mbali na wananchi 100 kupoteza maisha pia askari wawili waliuawa.
RPC KIGOMA
Akizungumza na MTANZANIA jana kwa njia ya simu, Kamanda Ottieno alisema
Zitto amezungumza upotoshaji na anatafuta umaarufu kupitia tukio hilo
hivyo apuuzwe.
“Zitto anazungumza upotoshaji, ni mwongo anatafuta kiki ambazo hazina
maana, wananchi wapuuze taarifa yake,”alisema Kamanda Ottieno.
Alipoulizwa endapo hakuna hata mwananchi mmoja aliyefariki katika
mapigano hayo, alisema ni wananchi wawili na askari wawili tu
waliopoteza maisha.
“Ni kweli askari wawili waliuliwa na jamii hiyo ya wafugaji katika
mapigano hayo na ni wananchi wawili tu ndiyo waliofariki na sio 100 kama
anavyopotosha Zitto,”alisema kamanda huyo.
Juzi gazeti hili lilizugumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi
Lugola ambapo alisema taarifa za wananchi 100 kuuawa si za kweli na
kwamba kwa sasa anasubiri taarifa kutoka kwa Inspekta Generali wa Jeshi
la Polisi (IGP), Simon Sirro.
“Sina taarifa za aina hiyo, lakini kuna askari wetu wawili walipoteza
maisha na IGP yuko kule tunasubiri atuletee taarifa,”alisema Lugola.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi, Zitto alisema wiki
iliyopita yalitokea mauaji ya askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la
Mto Malangarasi, Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza ambapo Mkuu wa Kituo
cha Polisi Nguruka aliuawa na wanaodaiwa kuwa ni wananchi wenye hasira.
“Tumekuwa tukifuatilia kwa kina yote yanayojiri huko Uvinza tangu kuuawa
kwa askari polisi wetu. Tunasikitika kusema kuwa taarifa tunazozipata
kutoka Uvinza zinaogofya mno.
“Kwani tunaambiwa kuwa wananchi zaidi ya 100 wa kabila la Wanyantuzu
wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi na polisi, wengine wakisema kuuawa
hata wakiwa kwenye matibabu hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye
purukushani na Jeshi la Polisi.
“Jeshi la Polisi limekalia kimya suala hili, pamoja na IGP kutembelea
eneo hilo la maafa. Haiwezekani kamwe tukio kubwa namna hii kutokea
halafu Serikali ibaki kimya bila kutoa maelezo yoyote kwa wananchi.
Uchunguzi wa kina unapaswa kufanywa ili kutambua nini kimetokea pale
Mpeta,”alisema Zitto.
Kutokana na hilo, alisema chama chao kinaendelea kukusanya majina na
taarifa za wote wanaodaiwa kuuawa na kitaweka wazi taarifa hizo.
Chanzo: Mtanzania
Social Plugin