
Picha haihusiani na habari hapa chini
Polisi wilayani Serengeti mkoani Mara wamekiri kumuua kwa kumpiga risasi, Edward Mahende (73) mkazi wa kijiji cha Kenyana A wakati wakisaka mtuhumiwa wa wizi wa mifugo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Juma Ndaki amesema tukio hilo limetokea Oktoba 12, 2018 saa 8 usiku nyumbani kwa marehemu.
Amesema Mahende alitoka na mkuki kwa lengo la kumchoma inspekta wa polisi aliyekuwa akipiga hodi katika nyumba hiyo.
Amesema marehemu alitoka akiwa na mkuki huo na askari walimshambulia kwa risasi na kufariki.
Na Anthony Mayunga, Mwananchi
Social Plugin