Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking : RADI YAUA WANAFUNZI SITA GEITA..YAJERUHI WALIMU NA WANAFUNZI KADHAA


Wanafunzi sita wa shule ya msingi, Emaco Vision iliyopo mjini Geita wamefariki dunia baada ya kupiga na radi wakiwa darasani huku wengine wakijeruhiwa wakiwamo walimu wawili.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Oktoba 17, 2018 saa 3:30 asubuhi. Wakati mvua ikinyesha na radi kubwa kupiga.

Ofisa elimu msingi, Yese Kanyuma amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema hadi sasa majeruhi ambao bado wako hospitali ni 25.

Hadi sasa wazazi wapo kwenye viunga vya hospitali ya mkoa wakisubiri taarifa za watoto wao wanaopatiwa huduma kwenye kitengo cha dharura hospitalini hapo.

Na Rehema Matowo, Mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com