Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana, Oktoba 22, 2018 amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali.
Taarifa ya ya Ikulu imeeleza kuwa Rais magufuli ameteua Wenyeviti watano kuchukua nafasi pamoja na kuziba nafasi za Wenyeviti wawili ambao wamekuwa wabunge.
Miongoni mwa walioteuliwa ni Dkt. Mwanza Kamata kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Biashara Tanznia (TANTRADE), akichukua nafasi ya Christopher Chiza ambaye amechaguliwa kuwa mbunge wa jiombo la Buyungu hivi karibuni.
Mwingine ni Dkt. Maria Mashingo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Maendeleo (TIB), akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Palamagamba Kabudi ambaye aliteuliwa kuwa mbunge na baadaye Waziri wa Katiba na Sheria.
Taarifa kamili kama ilivyoambatanishwa hapo chini.
Social Plugin