Uongozi wa Klabu ya Simba umeamua kufanya kisomo leo saa 8 mchana baada ya sala ya Ijumaa makao makuu ya Simba, Msimbazi kwa ajili ya kumuombea mwanachama wao Mohammed Dewji ‘MO’ aliyetekwa na watu wasiojulikana jana alfajiri.
Mo alitekwa jana Alfajiri alipokuwa anaenda kufanya mazoezi katika Gym za Hotel ya Colessum iliyopo, Osyterbay jijini Dar es Salaam.
Lengo la kisomo hicho kupitia taarifa ya Uongozi wa Simba, kumuomba Mwenyezi Mungu aweze kufanya wepesi kwenye matatizo yaliyompata mlezi na mwekezaji huyo.
MO ametekwa alfajiri ya jana Oktoba 11, katika hoteli ya Colosseumiliyopo Masaki, jijini Dar es salaam.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema idadi ya watu wanaoshikiliwa kwa mahojiano kuhusu tukio la kutekwa kwa MO Dewji, imefikia 12 hadi jana jioni.
Mambosasa alitaja idadi ya wafanyakazi watatu wa hoteli hiyo ndiyo wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.
"Kwa sasa wako 12 wakiwamo walinzi wote watano waliopo Kampuni ya G1 inayosimamia ulinzi wa hoteli hiyo, pia kuna Security Manager wa hoteli,"alisema Mambosasa.
"Uongozi wa Klabu ya Simba unapenda kuwataarifu Wanachama, Wapenzi na Washabiki wake kuwa mchana wa leo baada ya Sala ya Ijumaa (Saa 8.00) kutakuwa na *KISOMO* katika Makao Makuu ya Klabu Mtaa wa Msimbazi.
"Lengo la *KISOMO* hiki ni kumuomba Mwenyezimungu aweze kuleta wepesi kwenye Matatizo yaliyompata Mlezi na Mwekezaji wetu Bw. Mohamed Dewji “MO”
"Tunapenda kuwakaribisha katika Kisomo hiki muhimu ili kumuomba Mungu aweze kumlinda na kumrejesha Mwenzetu salama. *Tunatanguliza Shukrani*"-Taarifa ya Uongozi wa Simba
Social Plugin