Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TCRA YAWATAKA MA - ADMIN WA MAGROUP YA WHATSAPP KUWALEFTISHA WASIO NA MAADILI


Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imewaonya wasimamizi 'Admin' wa makundi ya Whatsapp yaliyoundwa kwenye simu za mkononi kwa kutosimamia maadili ya wanachama.


Makundi hayo ambayo huanzishwa kwa lengo mahususi yanatumika kama majukwaa ya mijadala,maelekezo ya kazi hata malumbano huku aliyeunganishwa akiwa na uhuru wa kujitoa kwenye kundi.

Onyo la TCRA dhidi ya wasimamizi wa makundi hayo limetolewa leo Oktoba 5 mjini Bukoba na ofisa wa mamlaka hiyo, Francis Mihayo wakati wa semina kwa viongozi wa mkoa wa Kagera.

Amewataka wasimamizi hao wa makundi hayo kutoogopa kuwaondoa wanachama wao wanaokiuka maadili kwa kuwa wao kama wasimamizi wanaweza kuchukuliwa hatua na mamlaka hiyo.


Na Phinias Bashaya,Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com