Na Leandra Gabriel,
IDADI ya vifo vilivyosababishwa na tetemeko la ardhi na tsunani nchini Indonesia vimefikia 832 huku vifo vingi zaidi vikihofiwa kuongezeka kadri maeneo yanavyofikiwa na waokoaji.
Mamlaka husika imetangaza kuwa wataanza kuzika miili hiyo iliyopatikana katika makaburi ya umma kwa kuhofia mlipuko wa magonjwa.
Aidha idadi kubwa ya watu wanasadikika kuwa hai chini ya vifusi, na katika mji wa Palu wamehitaji vifaa maaalmu ili kuweza kuwaokoa manusura waliokwama katika maduka na hoteli ambapo pamehofiwa kuhusu usalama kwa waokoaji hao.
Kwa upande wake wakala wa majanga nchini humo Sutopo Nugroho amevieleza vyombo vya habari kuwa ugumu katika vifaa (mashine za uokoaji) na mawasiliano ni changamoto kubwa ukilinganisha na idadi ya majengo yaliyoporomoka.
Tetemeko lenye ukubwa wa 7.5 lililikumba taifa hilo ikiwa ni miezi miwili tangu kutokea kwa tetemeko jingine na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa wa miundombinu.
Rais wa nchi hiyo Joko Widodo amekuwa akitembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika na kusaidia katika shughuli ya uokoaji na amekubali msaada wa kimataifa wa majanga kutokana na tetemeko hilo.
Social Plugin