Mshambuliaji
wa Ureno Cristiano Ronaldo, 33, amesema aliihama Real Madrid na
kujiunga na Juventus kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Uhispania
Florentino Perez hakumfanya ajihisi kama mchezaji anayethaminiwa na
kudhaminiwa sana. (L'Equipe, kupitia Express).
Real
Madrid wanamtaka meneja wa sasa wa Tottenham Mauricio Pochettino awe
meneja wao mpya wa kudumu kufikia mwisho wa mwezi huu. Miamba hao wa
Uhispania walimfuta kazi Julen Lopetegui baada yake kuhudumu kwa miezi
minne na nusu Jumatatu. Alifutwa baada ya Madrid kuchapwa 5-1 na
Barcelona Jumapili. (Sun).
Besiktas
wanataka kumrejesha kipa wa Liverpool Loris Karius kwa klabu hiyo ya
Anfield. Kocha huyo alitia saini mkataba wa mkopo wa miaka miwili na
klabu hiyo ya Uturuki.
Meneja
Jose Mourinho ataungwa mkono Januari kuwanunua wachezaji zaidi
kuimarisha kikosi cha Manchester United iwapo atawapata wachezaji
wafaao. Inadaiwa kwamba ametengewa kitita cha karibu £100m. (Guardian).
Mwanawe
Vichai Srivaddhanaprabha, Aiyawatt, aliyekuwa wa kwanza kumhoji meneja
Claudio Ranieri aliyewasaidia kushinda Ligi Kuu ya England kabla yake
kuteuliwa rasmi, anatarajiwa kuongoza Leicester baada ya babake kufariki
katika ajali ya helikopta iliyoua babake na watu wengine wanne. (Mail).
Mshambuliaji
wa Barcelona anayechezea Ufaransa Ousmane Dembele huenda akaruhusiwa
kuondoka klabu hiyo mwezi Januari. Chelsea, Liverpool na Arsenal ni
miongoni mwa klabu ambazo zimehusishwa na kutaka kumchukua mchezaji huyo
mwenye miaka 21. (Sun).
Juventus
wanataka sana kumnunua beki wa miaka 21 kutoka Serbia Nikola
Milenkovic, ambaye anadaiwa pia kunyatiwa na Tottenham na Manchester
United. Juve pia wanamtaka kiungo wa kati wa Italia Federico Chiesa, 21,
lakini Fiorentina huenda wakataka kulipwa zaidi ya euro 100m (£89m)
ndipo wakubali kuwaachilia wawili hao. (Calciomercato).
Meneja
wa zamani wa Aston Villa Steve Bruce anahusishwa na kuhamia Reading.
Klabu hiyo kwa sasa inashikilia nafasi ya 22 kwenye ligI ya wakiwa na
Paul Clement. (Birmingham Mail).
Meneja
wa Bournemouth Eddie Howe amemhakikishia mshambuliaji wa zamani wa timu
ya taifa ya England Jermain Defoe kwamba bado anahitajika Bournemouth,
licha ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 36 kuchezeshwa mara tatu pekee
Ligi ya Premia, wakati wote akiingia kama nguvu mpya. (Mirror).
Manchester
United hawajawasiliana na mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig Paul
Mitchell kuhusu kuhudumu katika nafasi kama hiyo ambayo wanapanga
kuianzisha Old Trafford. Hata hivyo, mkuu huyo wa zamani wa usajili wa
wachezaji Tottenham anafurahia kuhusishwa na kazi hiyo. (Sun).
Kiungo
wa kati wa Liverpool kutoka Brazil Fabinho, 25, anasema amekumbwa na
matatizo katika kujaribu kuzoea maisha mapya tangu alipohamia Anfield
kutoka Monaco kwa £39m majira ya joto. (ESPN).
Kutoka BBC