Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeyagawa ‘kimya kimya’ makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yaliyokuwa yakishikiliwa na mamlaka hiyo.
Septemba 5, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo alieleza kuwa iwapo uamuzi wa kuyagawa makontena hayo utafanyika, taasisi zitakazogawiwa zitajulikana.
Hata hivyo, wakati ikisubiriwa kujulikana kwa taasisi hizo, Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema tayari makontena yamekwishagawiwa.
Makontena hayo ambayo yalikosa wanunuzi katika minada yote mitatu iliyoendeshwa na kampuni ya udalali ya Yono yalikuwa na samani za viti, meza na mbao za kuandikia yakidaiwa kodi inayokadiriwa kufikia Sh1.2 bilioni.
Via>>Mwananchi
Social Plugin