Ronaldo alisaidia kupeleka mashambulizi yaliyokutana na Paul Dybala katika dakika ya 17 akimalizia kwa kupachika nyavuni bao lililodumu hadi kipyenga cha mwisho na kuifanya timu hiyo kuendelea kujikita kileleni kwa alama 5 zaidi ya Man Utd, ikiongoza Kundi H.
Mabingwa hao wa Italia walikuwa na nafasi kubwa ya kupachika magoli hasa katika kipindi cha kwanza ambapo walionekana kuwaelemea wapinzani wao kwa mbali, wakiwa na 70% za umiliki mpira (ball possession).
Hata hivyo, Manchester waliamka zaidi katika kipindi cha pili na kuanza kuwapa matumaini mashabiki wao, lakini hawakuonesha hatari kubwa langoni mwa Juve isipokuwa kwa mkwaju mmoja wa Paul Pogba uliomuelemea golikipa na kukutana na ‘mwamba’ wa goli.
Wababe hao watakutana tena Novemba 7 katika uwanja wa Allianz nchini Italia, Juventus itakapokuwa na faida ya kuwa mwenyeji.
Manchester imeendelea kushika nafasi ya pili katika kundi H, ikishukuru matokeo ya sare ya 1-1 kati ya Valencia na Young Boys waliocheza mapema hapa jana.
Social Plugin