Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ULAJI NYAMA UNABADILISHA HALI YA HEWA TANZANIA?


Minofu ya nyama ya ng’ombe tayari kwa kuandaliwa nyama ya kwenye makopo (beef production)


Na Andrew Kuchonjoma - Songea 

Ongezeko la watu Tanzania hivi sasa linasababisha mabadiliko ya hali ya hewa kutokana na ufugaji baada ya wananchi kuhamasika kufuga mifugo kwa ajili ya kitoweo.

Hayo yameelezwa na aliyewahi kuwa waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais serikali ya awamu ya nne Tanzania; aliyekuwa anashughulika na mazingira Dr. Teresya Luoga Huvisa ambaye pia alikuwa Rais wa baraza la Mawaziri wa Mazingira Afrika (President for African Ministers Council for Environment (AMCEN) katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi mapema wiki hii.

Dr. Huvisa alisema kwamba jambo hili hapa Tanzania kwa sasa linaweza kuchukuliwa kama mzaha lakini ndiyo ukweli kwamba ongezeko la watu linachangia uhitaji wa kula nyama kuwa mkubwa katika jamii na hivyo kusababisha kuongezeka kwa mifugo ambayo inachangia uharibifu wa mazingira kutokana na wafugaji kutafuta malisho ya mifugo yao pia kuchoma mkaa na kukata kuni kwaaajili ya kuchomea nyama mijini na vijijini.

Alisema kati ya nchi 209 Duniani, Tanzania ni ya 11 kuwa na mifugo mingi ambapo kwa mujibu wa shirika linaloshughulika na chakula duniani ( FAO); Tanzainia inakadiriwa kuwa na mifugo 24,531,673 kama vile ng’ombe, kondoo, mbuzi na nguruwe; na kwa Afrika ni nchi ya tatu kwani ya kwanza Ethiopia ina 54,000,000 na ya pili Sudani 41,917,000 ambapo takwimu zinaonyesha nchi zenye mifugo mingi maeneo yake yanakuwa jangwa kutokana na mazingirana kuharibiwa wakati wa malisho ya mifugo hiyo.

Alieleza kwamba sekta hiyo ya mifugo hapa Tanzania takwimu zinaonesha ni chanzo kizuri kinachochangia pato la nchi (GDP) kwani mwaka 2007 ilichangia asilimia 4.7, na 2009 ilikuwa asilimia 4.0 ambapo kwa ujumla wake mchango wa pato la Taifa, asilimia 40 ilitokana na uzalishaji wa nyama ya kusagwa “beef Production”. Ambapo takwimu hizo ni kwa mujibu wa wizara ya mifugo na uvuvi Tanzania kwa wakati huo kupitia taarifa zake za mwaka 2005.

Kutokana na uzalishaji nyama kiwandani lazima utatumika umeme unaotokana aidha na maji, gas, mwanga wa jua, mafuta ya dizeli (Industrial Diesel Oil) ambapo ukiacha maji na mwanga wa jua; nishati inayotokana na gas na dizeli ni chanzo kikubwa cha uzalishaji wa hewa za viwandani kama vile Methane na Kabonidayoksaidi (CO2) "Industrial Gases" ambazo huchangia kwenye ongezeko la joto duniani "Global Warming".

Dr. huyo alisema kwa kuwa ongezeko hilo linakwenda sambamba na ongezeko la watu hapa Tanzania wanaokadiriwa kuwa milioni 45 kwa mujibu wa sense ya mwaka 2012; hivyo hitaji la nyama linakuwa kubwa jambo ambalo linaongeza ari ya ufugaji hapa nchini pia ukataji wa misitu kwaajili ya kuni na uchomaji mkaa kwa ajili ya kuchomea nyama au kupikia unaongezeka na maeneo mengi yanaanza kuwa jangwa. 

Hivyo ongezeko la watu linasababisha hitaji la nyama kuwa kubwa na kadiri unavyokula nyama hasa mnofu ndivyo unavyoongeza utengenezwaji wa hewa ya kabonidayoksaidi (CO2) kwenye mwili wa binadamu ambayo hutolewa nje kama hewa chafu kwa njia ya kupumua na kujamba ingawa vitendo hivyo vyote ni kupumua. 

Alisema hewa hiyo ni hitaji la mimea ya kijani kibichi ambayo hutumika nyakati za mchana kujitengenezea chakula wakati wa fotosintesisi (photosynthesis) kwani wakati wa usiku mimea hiyo hutoa hewa ya CO2 nje kama hewa chafu wakati wa “respiration”na kuvuta hewa ya oksijeni (Oxygen). 

Alifafanua kwamba kujamba wengine wanaweza kucheka wakadhani ni kichekesho lakini hiyo ndiyo hali halisi kwani kinamchango katika uharibifu wa mazingira ikiwemo kuchangia kwenye ongezeko la joto Duniani “Global Warming linalosababishwa na kutobolewa kwa anga “Ozone layer depletion” inayochuja mionzi ya jua ili itue katika uso wa dunia kwa kiasi kwa lengo la kutoleta madhara kwa viumbe hai Duniani. 

Dr. alisema kwa mantiki hiyo uzazi wa mpango ni muhimu sana katika nchi yetu Tanzania na Duniani kwa ujumla wake, kwani kadiri watu wanavyokuwa wengi na ndivyo ulaji wa nyama unavyoongezeka na uharibifu wa mazingira ambao unaleta mabadiliko ya hali ya nchi unaongezeka ikiwa ni pamoja na joto kali, kuongezeka kwa kina cha bahari, mafuriko kutokana na mvua kubwa, matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwemo kansa ya ngozi, upofu wa macho (cataract) na hata kuzaliwa kwa watoto wa ajabu. 

Hivyo, kama misitu au mimea hiyo itatoweka maana yake hewa hiyo itakwenda moja kwa moja angani kupitia mionzi ya jua au mwanga wa jua. na hivyo kutoboa anga (ozone layer) kwa kusababisha matundu yanayopitisha mionzi ya jua bila kuchujwa na kutua kwenye uso wa dunia. 

Ongezeko la ulaji nyama hapa nchini kunaongeza mifugo hapa nchini na kusababisha mmomonyoko wa ardhi na kuuwa rutuba kwenye udongo kwani bacteria wanaohusika na utengenezaji wa rutuba ardhini “denitrifying” na “nitrifying bacteria” wanakuwa wameuawa kwa mionzi mikali ya jua linalotua moja kwa moaja ardhini. 

Lakini pia wadudu hao kukosa hewa kutokana na ardhi kuharibiwa na mifugo inayochungwa katika mashamba na misitu ambapo mapito ya mifugo hiyo mara kwa mara wanadhohofisha ardhi kwa kusababisha mmomonyoko wa udongo au udongo kushindwa kupitisha hewa kutokana na matundu ya udongo “air space” kujiziba. 

Kuuwawa kwa viumbe hivyo, muhimu hewa ya naitrojeni inayoongozana na mionzi ya jua haiwezi kubadilishwa na kuwa chakula cha mimea ya kijani kibichi wala ammonia ambayo hubadilishwa ardhini na kuwa tena hewa ya nitrogen ambayo inarudi tena hewani haiwezi kufanyika; kitendo ambacho kwa kitaalamu kinaitwa “Nitrogen Circle”. 

Kwa hiyo tatizo hilo ni hatari kwa afya ya binadamu kwa kuwa kama mimea ya kijani kibichi haitakuwepo hewa ya oksijeni (oxygen) inayotumika katika mfumo wa upumuaji kwa binadamu itapungua sana na hivyo kuathiri mifumo ya upumuaji na ikewezekana hata kusababisha vifo. 

Pia ardhi inakosa rutuba kwani bacteria hao wanachangia kwa kiasi kikubwa kurutubisha ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula. 

Dr. Huvisa alisema ili kuondoa au kupunguza tatizo hilo linalitokana na ulaji wa nyama inayotokana na mifugo nyumbani ni vyema kuunga mkono jitihada za serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ambayo imepiga marufuku kuchunga ama kuingiza mifugo, kukata miti na kuchoma mkaa katika maeneo ya misitu ya hifadhi ili kulinda uoto wa asili na ardhi. 

Lakini pia ingefaa sana hivi sasa kwa kuwa wananchi wanauhitaji mkubwa wa nyama na wanakula sana, kuangalia uwezekano wa kupunguza idadi ya mifugo kama inavyofanyika kwa binadamu kupitia uzazi wa mpango kwani uhitaji huo wa nyama unaongeza kwa kiasi kikubwa mifugo kwa wafugaji na wananchi kwa ujumla wake. 

Alisema mifugo inapoongezeka na hitaji la malisho linazidi kuhitajika, hitaji la nyama maeneo mengine ya nchi yanakuwa makubwa na ndio maana wafugaji wanaamua kuhamahama kufuata bei nzuri ya mifugo na nyama pia malisho baada ya kuharibu mazingira eneo la awali ambalo walikuwepo na hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira maeneo mengi. 

Ipo haja sasa kupima na kutenga maeneo kwaajili ya mifugo hiyo ya nyumbani kwa kila mkoa,wilaya, tarafa, vijiji ili iwe kama ilivyo kwa mifugo ya porini kwa lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira lakini pia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji hapa nchini. 

Mawasiliano: 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com