Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani akizindua umeme wa Rea
Waziri wa Nishati Dkt .Medard Kalemani katika akipiga ngoma mara baada ya kuzindua umeme wa Rea
Moja ya nyumba zilizowekewa umeme wakati wa uzinduzi huo
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza mara baada ya uzinduzi huo
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani mara baada ya uzinduzi huo
**
Waziri wa Nishati dk.Medard Kalemani amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya Umeme hasa vijijini ambapo gharama ya kuweka umeme ni shilingi 27000 katika vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi wa REA.
Dkt Kalemani ameyasema hayo wakati wa akizindua umeme katika kijiji cha Kikumbaitale wilayani Chato ambapo amesema serikali inakusudia kuipeleka Nchi katika uchumi wa Kati kupitia viwanda, hivyo amewataka wananchi wa Chato kuanzisha mashine za kukoboa na kusaga sambamba na kufanya biashara mbalimbali ikiwemo biashara za saluni.
Alisema uwepo wa umeme huo utakuwa fursa kubwa kwa wananchi kufungua biashara mbalimbali zitakazowaingizia kipato ikiwemo mashine za kusaga na kukoboa.
"Lakini pia niwaaambie pia fungueni na saluni kwani umeme huu muutumie kujiongezea kipato ambacho kitakuwa chachu ya kujiletea maendeleo katika eneo lenu “ alisema dkt kalemani na kuwapongeza viongozi wa TANESCO kwa kazi nzuri wanazofanya kwa kushirikiana na REA.
Hata hivyo alisema wataendelea kufanya kazi bila kuchoka kwa kutembelea vijiji mbali mbali ambavyo miradi ya REA inapita ili kukagua maendeleo ya mradi na kuhakikisha vijiji vyote vilivyo ndan ya mradi vinapata umeme kwa wakati.