Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WALIMU SABA WAFUKUZWA KAZI KWA UTORO IGUNGA


Na ABDALLAH AMIRI-IGUNGA

WALIMU saba katika shule mbalimbali za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wamefukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwamo utoro kazini.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juzi, Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wilaya ya Igunga, Hamisi Mpume, aliwataja walimu hao kuwa ni Paul Msabila aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Igunga mjini, Mary Elvance Kesi aliyekuwa akifundisha Shule ya Msingi Bulunde.

Wengine ni Lazaro Cheyo wa Shule ya Sekondari Nguvumoja, Leonard Chakupewa wa Shule ya Msingi Ziba, Rogasian Pacho wa Shule ya Msingi Nyandekwa, Sostenes Chiboko wa Shule ya Sekondari ya Sungwizi na Faustine Obadia wa Shule ya Msingi Ziba.

Alisema walimu hao walifikishwa katika tume ya utumishi wa walimu ya Wilaya ya Igunga na kubainika kuwa na makosa mbalimbali yakiwamo utovu wa nidhamu na utoro kazini kwa muda mrefu pasipo taarifa yoyote kwa mwajiri wao.

Mpume alisema pia wapo baadhi ya walimu ambao hakuweza kuwataja majina ingawa ameshapewa barua za onyo baada yakubaini makosa yao siyo yakufukuzwa kazi.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, ambaye pia ni Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Ntulila Hadoni, alisistiza taratibu zote za utumishi zimezingatiwa kabla ya kuchukuliwa uamuzi huo kwa mujibu wa sheria.
CHANZO- MTANZANIA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com