Watoto wawili waishio katika kijiji cha Mmart, wilaya ya Trans Mara Magharibi nchini Kenya wamedaiwa kupigwa na radi na kufariki papo hapo kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Watoto hao walipigwa na radi wakiwa wamelala nyumbani kwao kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Alhamisi ya wiki hii.
Tukio hilo pia lilipelekea majeruhi wawili, bibi mtu mzima pamoja na mwanamke mmoja wa makamo ambao wanaendelea na matibabu katika hospitali ndogo ya Emart inayopatikana katika eneo hilo.
Inadaiwa kuwa majeruhi hao walipoteza fahamu kufuatia mlio mkali uliotokana na radi hiyo na kulazimika kukimbizwa hospitali.
Wilaya ya Trans Mara inapatikana katika jimbo la Rift Valley, eneo ambako pia inapatikana mbuga kubwa na maarufu ya Masai Mara nchini humo, mbuga hiyo imefuata mkondo wa bonde la ufa lililoanzia nchini Tanzania.
Social Plugin