Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya siku nne mkoani Kagera ambapo atazindua miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu na afya katika wilaya za Kyerwa,Bukoba,Muleba na Biharamulo Karagwe sambamba na kuongea na wananchi katika mkutano wa adhara mjini Bukoba.
Akitoa taatifa hiyo kwa waandishi wa habari leo asubuhi ofisini kwake, Mkuu wa mkoa wa Kagera brigedia jenerali Marco Gaguti amesema waziri mkuu atawasili mkoani Kagera Oktoba 6 ambapo anatarajiwa kuhitimisha ziara yake Oktoba 9 mwaka huu.
Na Angela Sebastian- Malunde1 blog
Social Plugin