Chama cha waigizaji mkoa wa Kinondoni (TDFAA) kimemfungia mwanachama wake Wema Sepetu kujihusisha na masuala ya filamu kwa muda wa miaka miwili.
Huo ni mwendelezo wa adhabu kwa muigizaji huyo kufuatia kusambaa kwa video inayomuonyesha akifanya vitendo vinavyokinzana na maadili ya Mtanzania.
Chama hicho kimekwenda mbali zaidi na kutaka Mamlaka za kiserikali zipuuze utetezi unaotolewa na muigizaji huyo kwa kuwa una lengo la kuvipumbaza visimchukulie hatua.
Msemaji wa chama hicho Masoud Kaftany ameeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kamati ya maadili kujadili suala hilo kwa kina.
Amesema kamati imeunga mkono hatua zilizochukuliwa na bodi ya filamu na imeliomba Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kumuongezea adhabu itakayomzuia asijihusishe na shughuli zozote za sanaa kwa kipindi cha miaka miwili.
Social Plugin