Jebra Kambole, wakili wa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe anayeshikiliwa na polisi kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam, amesema mwanasiasa huyo amenyimwa dhamana.
“Polisi wamesema hawawezi kumuachia kwa leo wanaendelea kumshikilia kwa ajili ya mahojiano. Wamesema hawawezi kumpa dhamana,” amesema Kambole leo Jumatano Oktoba 31, 2018 wakati akizungumza na Mwananchi.
Zitto alikamatwa na polisi leo saa 5 asubuhi na kupelekwa kituo cha polisi Oysterbay ambako alihojiwa kwa takribani saa tatu, kisha kuhamishiwa kituo kikuu cha polisi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Liberatus Sabas leo amewaeleza wanahabari kuwa wanamshikilia Zitto kutokana na matamshi aliyoyatoa hivi karibuni.
Via Mwananchi
Social Plugin