Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE YAUA MWANAUME MBEYA

Leo November 7, 2018 Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limemkamata Theresia Venas Aisei kwa tuhuma za kumuua kwa kutumia kisu Viko Biko wa Iyela Jijini Mbeya.


Tukio hilo liligunduliwa na binti wa kazi Jenipher Salum Kihaga mapema asubuhi majira ya saa tano baada ya kumwita bosi wake kwa muda mrefu lakini hakuitika hali iliyomtia shaka na kuamuua kutoa taarifa kwa jirani ambaye ni mjumbe wa serikali ya mtaa Jesca Mwakalobo.

Hata hivyo wakiwa na mjumbe huyo walijaribu kumwita lakini hakukuwa na mwitikio ndipo walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa Mwalimu Simon Mwakaje ambaye alifika na alipofungua chumba alikuta marehemu ameuawa chumbani kwake huku chumba kikiwa kimetapakaa damu ambapo naye alitoa taarifa Polisi Mwanjelwa.

Polisi walifika eneo la tukio na kuufanyia uchunguzi wa awali na kisha kuupeleka mwili chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Kanda Rufaa Mbeya na kufungua jalada last uchunguzi namba MB/IR/10800/2018.

Awali Jesca alisema kwa mara ya mwisho majira ya usiku marehemu akiwa kwenye grocery yake alikuwepo mwanamke aliyekuwa amevaa hijabu au ushungi lakini hakumtilia shaka kwa kuwa alihisi ni mteja kama wateja wengine hivyo hakufanikiwa kumtambua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema tayari wamemkamata Theresia kupitia simu iliyokutwa chumbani kwa marehemu ambapo katika mahojiano mtuhumiwa amekiri kumuua marehemu akidai walifanya nae mapenzi lakini marehemu alitaka kumwingilia kinyume cha maumbile ndipo alikasirika na kuchukua kisu na kumchoma kichwani, ubavuni, mgongoni na tumboni.

Matei ametoa wito kuwa waangalifu na watu wasiowafahamu vizuri. Mtuhumiwa yupo mahabusu akisubiri kufikishwa mahakamani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com