Mtoto wa mwaka mmoja amenusurika kifo baada ya treni kumpitia juu yake alipokuwa ameangushwa kutoka mikononi mwa mama yake huko nchini India.
Mtoto huyo wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja aliyefahamika kwa jina la Sahiba aliponyeka kwenye ajali hiyo iliyotokea siku ya Jumanne katika kituo cha trani cha Mathura huku akiwa salama usalimini pasipo jeraha.
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni vimeripoti kuwa wazazi wa mtoto huyo wakiwa na watoto wengine wawili walifikwa na mkasa huo baada ya mtu mmoja kumsukuma mama na mtoto kudondokea kwenye njia ya treni wakati treni ikiwa kwenye spidi na kupita juu yake.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha The Times of India, baba wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Sonu amesema waliposhuka kwenye treni, mke wake akiwa amembeba ‘Sahiba’ alisukumwa na mtu na kupelekea kuanguka kwenye njia ya treni.
Asif Khan akiwa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo amesema kuwa wakati akisubiria treni kuelekea Nagpur ghafla akaona mtoto akianguka na hata baada ya kupita kwa treni hakuna aliyeamini kuwa ni mzima wa afya na asiyekuwa na majeraha.
Mara baada ya tukio hilo kilammoja aliyekuwepo mahala hapo alihitaji kumshika mtoto huyo na kumuombea kwani ilikuwa kama miujiza kwa mtoto huyo kupona katika ajali hiyo huku akiwa hana hata majeraha.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Social Plugin