Moja ya gari lililopata ajali na kuteketea kwa moto Tarime.
Takribani watu 15 wamefariki dunia baada ya kuteketea kwa moto kufuatia ajali iliyotokea katika eneo la Komaswa maarufu kama kwa Gachuma lililopo wilayani Tarime mkoani Mara kwa kuzikutanisha gari mbili za abiria aina ya Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na kisha kuteketea kwa moto.
Henry Mwaibambe, kamanda wa jeshi la polis kanda maalum Tarime Rorya akizungumza akiwa katika eneo la tukio ameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa bado hakijajulikana lakini dereva wote kwenye ajali hiyo wamepoteza maisha.
“Kuna watu wengine ambao hawajatambuliwa, tunajitahidi ili watambuliwe, chamsingi ambacho hakina ubishi madereva wote wamefariki, lakini tunaendelea na uchunguzi ili kujua idadi kamili ya watu waliofariki hatuwezi kuwaficha marehemu,” amesema Kamanda Mwaibambe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Tarime Bw. Glorius luoga ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kuwataka madreva kuwa makini pindi wanapokuwa wamebeba abiria kwenye vyombo vyao vya usafiri.
Social Plugin