Mwita Waitara kushoto na Rais Magufuli kulia
Ikiwa siku 4 zimepita tangu kuapishwa bungeni kwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, Rais John Magufuli leo Novemba 10, 2018, amemteua kuwa Naibu waziri katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri aliyoyafanya.
Mwita ambaye alichaguliwa kuwa mbunge wa Ukonga katika uchaguzi mdogo uliofanyika Septemba 16, 2018, ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa TAMISEMI akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Mh. Joseph Kakunda ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa Viwanda.
Mwita Waitara aliyejiuzulu ubunge kupitia CHADEMA katika jimbo hilo hilo na kuhamia CCM ambako alipata nafasi ya kugombea na kushinda kiti hicho tena, ameapishwa bungeni Novemba 6, 2018, hivyo ameteuliwa ndani ya siku 4 akiwa kama mbunge.
Katika mabadiliko hayo madogo kwenye Baraza la Mawaziri Rais Magufuli pia ametengua uteuzi wa Waziri wa Viwanda Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Kilimo Charles Tizeba.
Social Plugin