Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking : AMBER RUTY NA WASHIKAJI ZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA VIDEO ZA NGONO


Mcheza video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty) (hayupo pichani) wakiwa kwenye moja ya chumba cha Mahakama mara baada ya kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kuzisambaza mitandaoni.
Mshtakiwa Amber Ruty wa kwanza kulia anayedaiwa kupiga naye Picha kinyume na maumbile, Said Mtopali pamoja ma James Charles maarufu kama James Delicious wakiwa nje ya chumba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashtaka yao.
Picha na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
 ***
Mcheza video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty) na kijana James Charles maarufu kama James Delicious anayedaiwa kuwa shoga wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kuzisambaza mitandaoni.

Washitakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Novemba 2,2018 kwa ajili ya kusomewa mashtaka juu ya kesi inayowakabili ya kusambaza video zenye maudhui ya ngono mtandaoni.

Akiwa mahakamani hapo, Amber Rutty amesomewa mashtaka mawili, moja la kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile na kosa la pili ni kusababisha kusambaa kwa picha za ngono.

Wakati huo huo kijana anayejulikana kwa jina la James delicious naye amepandishwa mahakamani na kusomewa shtaka moja la kusambaza video za ngono mtandaoni, ambapo amekataa shtaka hilo.

Ifahamike kuwa iwapo watuhumiwa hao watakutwa na hatia juu ya makosa yao, kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watalazimika kwenda jela maisha au adhabu isiyopungua miaka 30 jela.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com