Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HATIMAYE AMBER RUTY NA MPENZI WAKE WAPATA DHAMANA


Video vixen, Nascat Abdul maarufu kama Amber Ruty sambamba na Mpenzi wake Saidi Bakari Kitomali, hatimaye wamepata watu wa kuwatolea dhamana, juu ya kesi yao inayowakabili.

Dhamana hiyo imetolewa leo, Novemba 27 ambapo Amber Rutty amedhaminiwa na ndugu yake, huku mpenzi wake akidhaminiwa na Mchungaji Daudi Mashimo wa Kanisa la Emmaus Bible Church, Mbezi Luis Dar es salaam.

Hapo jana Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwezire alisema dhamana ya wawili hao bado iko wazi, ambapo ilikuwa ikihitaji wadhamini ambao kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 15, wawe na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati za kusafiria, pia wasitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.

Ikumbukwe kwamba Mchungaji Daudi Mashimo ndiye aliyetangaza kufanya maombi maalum kwa Wema Sepetu, na kumtaka muigizaji huyo kuokoka ili kuondokana na mikosi inayomkabili katika maisha yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com