Kama ukiangalia katika simu yako nina uhakika Application nyingi ulizopakua ni za bure.Wote tunapenda App za bure.
Mara nyingi App za bure zina gharama ya faragha (privacy) wakati wa kuziingiza katika kifaa chako.
Je unasomaga vigezo na masharti kabla ya kuipakua hiyo Application na kuiweka kwenye simu yako? Ninauhakika jibu na HAPANA.
Wengi huwa tunabonyeza tuu ‘Agree’ katika vigezo na masharti, kitu ambacho ni kosa kubwa.
Lazima usome kuwatambua waliotengeneza na ujue ni vitu gani unawaachia mikononi mwao kama vile namba za simu, meseji zako, maeneo (locations) na vitu vingine kibao.
Tuende moja kwa moja kwenye mada ya leo.Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wataalam waliobobea wa kituo cha ESET umebaini uwepo wa Application 29 zilizopo Google Play Store ambazo ni VIRUSaina ya TROJAN
Kwa mujibu wa utaifiti huo, virusi hao ambao hutumia majina tofauti tofauti wanauwezo wa kuingilia application zingine zilizopo katika simu yako na kutuma taarifa zote kwa Hackers(Wadukuzi).
App hizo ambazo zina virus ndani yake, pia zinauwezo wa kutengeneza Fake Logins Page ( Phishing) ambapo ukijichanganya tu basi taarifa zako za siri kama bank details,email, password zako za mitandao ya kijamii huchukuliwa na kutumwa kwa Hackers.
==>Baadhi ya App hizo ni:
Daily Horoscope – Astrological Forecast
Master Cleaner – CPU Booster
Speed Cleaner – CPU Cooler
Master Clean – Power Booster
Horoscope 2018
Super Fast Cleaner
Ni imani yangu makala hii imekufungua macho na utakuwa makini zaidi ili kujikinga na wadukuzi wa mitandaoni.
<<INGIA HAPA>> Kuzijua App zote 29 ambazo zina virusi ndani yake. Kama ulizipakua basi zifute kabisa kwenye simu yako.
Social Plugin