Jumuiya ya wahitimu ya Chuo Kikuu Ardhi (Adhi University Convocation) jana imefanya matembezi ya hisani yenye lengo la kuwaita wanajumuiya wote wa chuo hicho (ALUMN) ili kukumbuka nyumbani (waliposoma) hivyo kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo za chuo.
Maandamano yaliongozwa na Rais wa baraza la wahitimu la Chuo hicho, Haruna Masebu pamoja na Naibu makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala, Profesa Robert Kiunsi.
Mbali na matembezi hayo kulikuwa na mazoezi ya ya pamoja na michezo mbalimbali kiwemo Aerobic, Soka na mbio.
Miongoni mwa washiriki walikuwepo pia sehemu ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ALUMNI wakiongozwa Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Maulid Bajani.
Pia alikuwepo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Dkt. Moses Kusiluka ambaye ni mdau mkubwa wa chuo hicho.
Wengine ni UCLAS Veteraniambao walicheza soka na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi na kuibuka kidedea.
Sehemu ya wadau (ALUMN) na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) pamoja na wadau wao Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakifanya matembezi katika Barabara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Novemba 24, 2018 kwa ajili ya shughuli za chuo jijini humo. Chuo hicho kinatarajiwa kuwa na Kongamano la wahitimu (CONVOCATION) Ijumaa ya Novemba 30, 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
Sehemu ya wana ALUMNI na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifanya matembezi katika Barabara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Novemba 24, 2018.
Sehemu ya wana ALUMNI na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifanya matembezi katika Barabara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Novemba 24, 2018.
Sehemu ya wana ALUMNI na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifanya mazoezi ya viungo baada ya matembezi hayo.
Sehemu ya wana ALUMNI na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifanya mazoezi ya viungo baada ya matembezi hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Sophia Kongela (tisheti ya blue) akiwa katika picha pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kushiriki matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Pamoja naye (wa saba kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dkt. Maulid Banyani.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Maulid Banyani akitoa agizo kwa wafanyakazi wa shirika hilo kuanzia sasa kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi pamoja mara moja kila mwezi baada ya kushiriki matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu Ardhi (ARU). Mwenye (tisheti ya blue) ni Mwenyekiti wa NHC, Dkt. Sophia Kongela.
Social Plugin