Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE BITEKO ACHANGIA MIRADI YA MAENDEO JIMBONI BUKOMBE


Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM), ameunga mkono juhudi za maendeleo za wakazi wa Kata ya Namonge jimboni humo kwa kuchangia utekelezaji
wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na wakazi hao.


Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Shilabela Novemba 03, 2018, Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini alichangia mifuko 30 ya
saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Shilabela pamoja na shilingi laki nane kwa ajili ya ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi
Nyamagwangala.

Biteko alitumia mkutano huo kuwapongeza wananchi wa Jimbo la Bukombe kwa kubuni na kutekeleza miradi
mbalimbali ya ya maendeleo na kwamba serikali itaendelea kuwaunga mkono kwani maendeleo ni ushirika baina ya serikali na wananchi.


Na George Binagi-GB Pazzo 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini, akizungumza na wakazi wa Kata ya Namonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Shilabela.

Tazama Video hapa chini




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com