Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI KUU YA TANZANIA 'BOT' YAZIFUNGIA BENKI TANO

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezifungia kwa mwezi mmoja benki za kibiashara tano kutojihusisha na ubadilishaji wa fedha za kigeni kutokana na sababu ambazo bado hazijawekwa wazi.


Hatua hiyo ya BoT inatazamwa kama mwendelezo wa chombo hicho kikuu cha usimamizi wa fedha kudhibiti biashara ya utakatishaji na ubadilishaji wa fedha kiholela.

Takriban wiki mbili zilizopita BoT iliyafungia maduka kadhaa jijini Arusha kwa madai kuwa yanaendesha shughuli zake kinyume na sheria zinazosimamia biashara hiyo, baada ya hapo ilitangaza kuwa huduma za ubadilishaji fedha zitapatikana katika hoteli za kitalii, benki na ofisi zao.


Kwa mujibu wa taarifa ya BoT, benki zilizofungiwa kufanya biashara ya ubadilishaji fedha kuanzia Novemba 23 ni Barclay, Exim, UBA, ABC na Azania.


“Hatua hii imetokana na kuvunjwa kwa taratibu na kanuni, waliofungiwa walikuwa aidha wanafanya biashara kinyume na viwango vinavyowekwa au walikuwa hawawasilishi taarifa za miamala waliyokuwa wanafanya,” alisema Alexander Mwinamila ambaye ni mkurugenzi wa masoko ya fedha wa BOT.


Aliongeza kuwa hatua iliyochukuliwa inalenga kusimamia kanuni na taratibu za soko la ubadilishaji fedha za kigeni kwa mujibu wa sheria za nchi hii.


Barclays Tanzania na Exim Wametoa ufafanuzi hapo chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com