Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DR. FEKI ALIYETOROKA MAHAKAMANI ADAKWA TENA KWA KUJIFANYA DAKTARI DODOMA

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Hassan Abdallah Athuman, umri miaka 38 kwa tuhuma za kujifanya Daktari wa magonjwa ya binadamu bila kuwa na vibali maalum.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Gilles Muroto amezungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo Novemba 24, 2018.

RPC Muroto amesema; “Huyu tumemkamata eneo la Kijiji cha Mwakisabe alikuwa akitoa Taaluma ya Utabibu bila ya kusomea ni Daktari feki, huyu aliwahi kukamatwa huko nyuma kwa kosa kama hili, alitoroka Mahakamani”


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com