DC KIZIGO AMTAKA MGANGA MKUU WA WILAYA KUAGIZA DAWA KWA WAKATI

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo amemuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha kabla dawa kumalizika kabisa awe ameshaagiza zingine ili ziwepo wakati wote.

Kauli hiyo, ameitoa leo wakati alipokuwa katika ziara katika kata za Rwinga na Namtumbo kwa ajili ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kusikiliza kero za wananchi.

Aidha ameagiza pia ahakikishe anaagiza dawa zinazotosha kata mbili (Rwinga na Namtumbo) kwani ni dhahiri kituo kinazidiwa na idadi ya wagonjwa kwani kinahudumia kata 2 badala ya 1.

"Kuhusu matumizi ya computer, Nimeagiza Mganga Mkuu wa wilaya ahakikishe mafunzo kwa vitendo yanatolewa na kufanyika ili kuongeza kasi ya watumishi kuhudumia watu kwa kutumia computer kwani bado hawajazizoea katika kufanya kazi zao", amesema Kizigo.

Hata hivyo, amesema endapo kutakuwa kuna mgonjwa ambaye amezidiwa waweke kipaumbele katika kumhudumia hata kama hawajamaliza kuingiza taarifa kwenye computer.

Kizigo amesema kufuatia kero ilioyotolewa na wananchi kutoza flat rate shilingi 7000 kila mwezi kwa wananchi kulipia maji, wakati maji yanatoka mara 1 kwa wiki inayopelekea maji kutoka mara 4 tu kwa mwezi, ameiagiza idara ya maji iwaandikie EWURA kuomba kuletewa mita za maji haraka ili wananchi walipe kwa haki kutokana na maji wanayoyatumia.

"Licha ya Mkuu wa idara ya maji kutoa majibu kwamba wanatoza 7000 flat rate kwa sababu hakuna mita za maji katika baadhi ya maeneo, nimesema hii sio haki kuwalipisha shilingi 7000 kwa kuchota maji mara 4 tu kwa mwezi tena kwa uchache ", amesema Kizigo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post