Na Imma Msumba Arumeru
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kwa kushirikiana na Jeshi la polisi Wilaya ya Arumeru limewakamata watuhumiwa wa Tatu ambao wameshiriki kumtoa mimba mwanafunzi wa kidato cha nne kwa kutumia dawa za miti shamba suala ambalo linachochea mimba kwa wanafunzi na kuzorotesha elimu yao.
Dc Muro amesema kuwa wamebaini tukio hilo baada ya kuweka mtego na kuwabaini watuhumiwa hao pamoja na mtia mimba ambao wamefikishwa polisi kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
Akielezea jinsi alivyopewa ujauzito na kisha ujauzito kutolewa aikaeli Pallangyo amesema ni kweli alipata ujauzito Kwa kurubuniwa na kijana wanaeishi nae Jirani nyumbani ambae alikuwa akimrubuni kwa kumpatia fedha.
Kwa upande wao watuhumiwa wa sakata hilo kijana aliempa mimba Binti,pamoja na mama Mzazi wa Aikaeli na mwanamke ambae ni ndugu wa Kijana aliempa mimba ambae anatajwa kuhusika na kumtoa ujauzito Binti wametoa sababu mbalimbali ambazo hata hivyo zimeonekana kukinzana zenyewe Kwa zenyewe Kutokana na mama wa Binti kukiri Kuwafahamu watuhumiwa wenzake na kuelezea tukio la Mchezo mzima ulivyokuwa.
Akidhibitisha taarifa za Binti huyo kuwa mjamzito na kutoa ujauzito, Mganga mkuu wa halmashauri ya Meru Daktari Cosmas kilasara amesema vipimo vya awali vilionyesha Binti kuwa mjamzito na vipimo walivyofanya tena vimeonyesha Binti sio mjamzito tena ambapo amesema hata hivyo Binti huyo ameendelea kupata dalili zote za kuwa na ujauzito ikiwemo ya maziwa kutoka.
Kutokana na tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amevigiza vyombo vya Usalama kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote ambao wamehusika katika tukio hilo , ambapo pia amelitaka jeshi la Polisi kuhakikisha wanawakamata na wanawafikisha mahakamani watu wote waliohusika katika kuwapa ujauzito wanafunzi 57 Kwa kipindi Cha miaka miwili iliyopita.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru