Mbali na Amber Ruty washtakiwa wengine ni Said Bakary Mtopali na James Charles maarufu kama ‘James Delicious’.
Kwa pamoja washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwezire na wakili wa serikali Nassoro Katuga.
Wakili Katuga amedai kuwa kosa la kwanza ni kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo linamkabili Amber Ruty.
Inadaiwa ametenda kosa hilo kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary Mtopali kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.
Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary Mtopali ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Ruty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.
Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.
Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruty na Said Abubakary Mtopali ambapo wanadaiwa kati October 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Katuga amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wanasubiri taarifa za Kitaalamu kuhusu picha hizo za ngono za minato.
Washtakiwa wamepatiwa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini 2 kila mtu na kusaini bondi ya Shilingi Milioni 15.
Pia wadhamini wawe na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zao za kusafiria na wasitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.
Hata hivyo mshtakiwa James Delicious aliyefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana, huku Amber Ruty na Said Bakary Mtopali wameshindwa kutimiza masharti na kupelekwa gerezani.Kesi imeahirishwa hadi November 12,2018.