Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKUU WA MKOA AZUNGUMZIA DUDE LILILOZUA BALAA KAGERA

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema wanaendelea kufanya mawasiliano na wataalamu wa jiolojia ili kubaini ni kitu gani kilichotokea usiku wa kuamkia leo
kilichosababisha kishindo kikubwa kilichoambatana na muungurumo mkubwa na mwanga mkali.


Tukio hilo limetokea jana majira ya kati ya saa tatu na tatu na nusu, kilisikika kishindo na muungurumo mkubwa na kusababisha taharuki kwa wakazi wa mkoa wa Kagera, uliotokana na wengi kudhani ni tetemeko la ardhi.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Gaguti amesema pia wanafanya mawasiliano na viongozi walioko katika wilaya mbalimbali ili kubaini kama kuna wananchi wamesikia jambo hilo kwa ukaribu zaidi ili kupata pa kuanzia kufanya uchunguzi wa kina.

“Tunaendelea kuwasiliana na wataalamu wa jiolojia,ili wafanye kufanya utafiti wao kwa kutumia vifaa vyenye viwango vya juu zaidi na baadae tutapata mrejesho kama ni kimondo au ni kitu kingine kinachofanana na hicho” alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com