Mwaandishi wa habari kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo Bw.Mussa Yussuph akifanya mahojiano na Mkuu wa Idara ya Kemia katika Shule ya Sekondari Viwandani, Mwalimu Projestus Kabagambe, wakati akielezea uchambuzi wa kitabu chake kuhusu utumishi wa Rais Dk. Magufuli katika miaka mitatu tangu alipoingia madarakani Jijini Dodoma
Mkuu wa Idara ya Kemia katika Shule ya Sekondari Viwandani, Mwalimu Projestus Kabagambe, akielezea uchambuzi wa kitabu chake kuhusu utumishi wa Rais Dk. Magufuli katika miaka mitatu tangu alipoingia madarakani Jijini Dodoma
Mkuu wa Idara ya Kemia katika Shule ya Sekondari Viwandani, Mwalimu Projestus Kabagambe, akionesha kitabu chake mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa uchambuzi wa kitabu chake kuhusu utumishi wa Rais Dk. Magufuli katika miaka mitatu tangu alipoingia madarakani Jijini Dodoma
Mkuu wa Idara ya Kemia katika Shule ya Sekondari Viwandani, Mwalimu Projestus Kabagambe, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) wakati akielezea uchambuzi wa kitabu chake kuhusu utumishi wa Rais Dk. Magufuli katika miaka mitatu tangu alipoingia madarakani Jijini Dodoma
............................
Na Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma
SerikaliI imeshauriwa kubadili mfumo wa elimu kuwawezesha wahitimu katika ngazi mbalimbali za kitaaluma waweze kujitambua na kujitegemea ili kuendana na kasi ya mageuzi ya kiuchumi yanayofanywa na Rais Dk. John Magufuli.
Akitoa ushauri huo mbele ya waandishi wa habari Mkuu wa Idara ya Kemia katika Shule ya Sekondari Viwandani, Mwalimu Projestus Kabagambe, wakati akielezea uchambuzi wa kitabu chake kuhusu utumishi wa Rais Dk. Magufuli katika miaka mitatu tangu alipoingia madarakani.
"Rais amekuwa akisisitiza umuhimu wa taifa kujitegemea na ndivyo hivyo hata mfumo wetu wa elimu unapaswa pia kubadilishwa ili uwe wa kumfanya muhitimu aweze kujitambua na kujitegemea.
Mwalimu Kabagambe amesema mfumo wa elimu uliokuwepo katika kipindi cha Azimio la Arusha mwaka 1967, ulimwezesha mwanafunzi katika kila ngazi ya elimu kuwa na uwezo mzuri wa kuitumikia jamii, lakini sasa wahitimu wamekuwa tegemezi zaidi.
Hata hivyo Mwalimu Kabagambe ameelezea kuwa ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiuchumi ambayo Rais Dk. Magufuli amekuwa akiisisitiza ni muhimu mfumo wa elimu ukawajenga vijana kubaidili fikra za utegemezi na wawe wachochezi kwenye mapinduzi ya kiuchumi.
Amesema kuwa mabadiliko ya mfumo wa elimu yaliyofanyika mwaka 2005 kwa lengo la kumjengea umahili wa kitaaluma mwanafunzi, bado haujaleta manufaa, hivyo unahitaji mabadiliko.
Kabagambe amesema kuwa kupitia kitabu hicho kiitwacho "Rais abomoa hekalu na kulijenga upya" ameelezea mageuzi ya kiuchumi yaliyofanywa na Dk. Magufuli, ambayo yatabaki kuwa historia ya kutukuka kwa vizazi vijavyo.
"Muhimu tukawaeleza wananchi wenzetu mambo muhimu yaliyofanyika ndani ya miaka mitatu, hekima ya Rais katika kuwatumikia wanyonge, imeifanya Tanzania kuwa taifa jipya.
Na pia ameelezea kuwa Utendaji wake umeakisi ahadi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wananchi kupitia Ilani ya uchaguzi pamoja na kukidhi matakwa ya kikatiba ya CCM.
Mwalimu huyo ambaye pia ni mwandishi wa vitabu vya kemia vya kidato cha kwanza hadi cha sita, alisema kupitia kitabu hicho chenye sura 13, ameelezea namna ambavyo utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama ujenzi wa reli ta kisasa, bomba la mafuta, ununuzi wa ndege utakavyolinufaisha taifa kiuchumi
Social Plugin