Shule ya Sekondari Kom ‘Kom Secondary’ iliyopo eneo la Butengwa mjini Shinyanga imefanya Mahafali ya Kumi ambapo Jumla ya wanafunzi 180 wamehitimu masomo yao ya kidato cha nne mwaka 2018.
Mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 10 ya Kom Sekondari iliyoanzishwa mwaka 2006 yaliyofanyika leo Jumamosi Novemba 17,2018,alikuwa Meneja wa Benki ya CRDB Shinyanga,Said Pamui.
Awali akizungumza,Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari Jackton Koyi alisema anaamini wanafunzi wake watafanya vizuri kwenye mitihani yao kwani walijiandaa vizuri na mazingira ya kujifunzia shuleni ni rafiki kwa wanafunzi.
“Mwaka huu wahitimu ni wengi sana ukilinganisha na miaka mingine ambapo wahitimu walikuwa hawafiki 150 lakini leo wanahitimu 180,tunawashukuru wazazi na walezi kwa kuendelea kutuamini kuwa walezi wa watoto wenu,lakini pia tunaishukuru benki ya CRBD wamekuwa wadau wazuri kwa shule yetu”,alisema Koyi.
Naye Mkuu wa shule,Mwita Warioba alizitaja changamoto zilizopo shuleni hapo kuwa ni pamoja na baadhi ya wazazi kutohudhuria vikao vya shule,wanafunzi kuchelewa kufika shuleni kutokana na baadhi ya wazazi kutowalipia ada wanafunzi lakini pia baadhi ya wazazi wamekuwa wagumu kuwalipia bima za afya watoto wao.
Mgeni rasmi,Saidi Pamui alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wazazi na walezi kuwakatia bima za afya wanafunzi ili waweze kupata matibabu kwa gharama nafuu wanapougua pamoja na kuwawekea akiba benki kwa kuwafungulia ‘Junior Jumbo account’ katika benki ya CRDB.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa mahafali hayo,ametusogezea picha 71 za matukio yaliyojiri...Tazama hapa chini
Mgeni rasmi,Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Saidi Pamui (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali na wahitimu 180 wakiandamana wakati wa Mahafali ya 10 ya Kom Secondary leo Jumamosi Novemba 17,2018 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa shule ya sekondari Kom Mwita Warioba (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa shule hiyo Jackton Koyi (wa pili kulia) wakimwongoza mgeni rasmi Said Pamui kuelekea kwenye ukumbi wa mahafali ya 10 ya Kom Secondary.
Katikati ni Magreth Koyi (mke wa Jackton Koyi ambao ni wamiliki wa shule ya 'Kom Secondary',kulia ni mdau wa Kom Secondary bwana Jomba,Kushoto ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule wakiwa kwenye maandamano.
Mgeni rasmi Said Pamui akikata utepe wakati wa mahafali ya 10 ya Kom Secondary.
Wahitimu wa kidato cha nne 2018 wa shule ya sekondari Kom wakiwa kwenye maandamano kuelekea ukumbini.
Wahitimu wakiingia ukumbini.
Bendi ya shule ya Kom Sekondari wakati wa kuimba wimbo wa Tanzania.
Sehemu ya Wahitimu wakiwa wamesimama.
Wahitimu wa kidato cha nne wakiwa wamesimama.
Wahitimu wakiwa eneo la tukio.
Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari Jackton Koyi akizungumza wakati wa mafahali ya 10 ya kidato cha nne mwaka 2018.
Wazazi na walezi wa wanafunzi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari Jackton Koyi akizungumza wakati wa mafahali ya 10 ya kidato cha nne mwaka 2018.
Mgeni rasmi ,Said Pamui akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya 10 ya kidato cha nne Kom Secondary mwaka 2018.
Mgeni rasmi,Said Pamui akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha nne Kom Secondary wakikata keki maalumu ya shukrani.
Wahitimu wa kidato cha nne 2018 Kom Secondary wakilishana keki.
Mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kidato cha nne 2018 Kom Secondary 2018,Said Pamui akilishwa keki.
Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari Jackton Koyi akijiandaa kula keki.
Walimu shule za Kom Sekondari na Msingi wakicheza wakati wa mahafali ya 10 ya kidato cha nne 2018 Kom Secondary.
Wahitimu ,Salma Shaaban na Raphael Jeremiah wakisoma risala.
Vijana wa Skauti wakijiandaa kuonesha maonesho mbalimbali.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali.
Vijana wa Skauti wakionesha ukakamavu.
Wanafunzi wa Kom Sekondari wakitoa burudani ya Vichekesho kwa njia ya taarifa ya habari.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Kom, Peter Kuguru akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Wazazi na walezi wa wanafunzi wakiwa kwenye mahafali.
Wazazi na walezi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mahafali yanaendelea.
Mahafali yanaendelea.
Wanafunzi wa Kom Secondary wakionesha ubunifu wa mavazi ya kabila la Kimasai.
Wazazi na walezi wakifuatilia maonesho ya ubunifu wa mavazi.
Mbunifu wa mavazi ya asili akicheza wimbo wa Saida Karoli.
Wazazi na walezi wakifurahia burudani.
Wanafunzi wa Kom Secondari wakiwa wamevaa mavazi ya aina mbalimbali wakati wa onesho la ubunifu wa mavazi.
Wazazi wakifuatilia burudani.
Vijana wa maonesho ya ubunifu wa mavazi wakiondoka ukumbini.
Wazazi wakifuatilia matukio.
Mahafali yanaendelea.
Wazazi wakiwa eneo la tukio.
Mahafali yanaendelea.
Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio.
Wanafunzi wa Kom Secondary wakiruka sarakasi.
Vijana wakiruka sarakasi.
Meza kuu wakifuatiliaa burudani.
Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Shinyanga,Said Pamui akizungumza wakati wa harambee kuchangia ujenzi wa nyumba ya Mlezi wa wanafunzi wa Kom secondary (Matron) iliyofanyika wakati wa mahafali ya 10 ya kidato cha nne 2018.
Akina mama wakiwa mstari wa mbele kabisa wakati wa harambee hiyo.
Akina mama wakishikana mkono na mgeni rasmi na kuchangia wakati wa harambee hiyo.
Akina mama wakiwa kwenye foleni kwenda kutoa michango yao na kushikana mkono na mgeni rasmi.
Akina baba nao hawakuwa nyuma kuchangia wakati wa harambee...nao wakajitokeza kwa wingi.
Akina baba wakiendelea kutoa michango yao na kushikana mikono na viongozi mbalimbali wakati wa mahafali hayo.
Mahafali yanaendelea.
Walimu wa shule za Kom wakiwa kwenye mahafali
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali.
Wazazi wakiwa eneo la tukio.
Wanafunzi wanaobaki wakiimba shairi.
Mgeni rasmi,Said Pamui akizungumza wakati akijiandaa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne Kom Secondary 2018.
Mhitimu,Rajuu Masoud ,bingwa wa uchoraji akijiandaa kupokea cheti cha pongezi pamoja fedha taslimu shilingi 20,000/-
Zoezi la kukabidhi vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye michezo,usafi,nidhamu na taaluma likiendelea.
Zoezi la kukabidhi vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye michezo,usafi,nidhamu na taaluma likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi kwa mabingwa wa masomo likiendelea.
Mwanafunzi bingwa wa somo la Kiswahili akipokea cheti.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali.
Wahitimu wa kidato cha nne Kom Secondary 2018 wakiwa kwenye foleni kupokea vyeti.
Wahitimu wa kidato cha nne wakiwa kwenye foleni wakisubiri kukabidhiwa vyeti.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Wahitimu wa kidato cha nne Kom Secondary wakiendelea kupokea vyeti.
Social Plugin