Polisi katika Kaunti ya Bungoma nchini Kenya wameanzisha upelelezi kujua namna binti mwenye umri wa miaka 15 alivyofia mikononi mwa wazazi wake.
Majirani wanadai binti huyo aitwaye Abigael Namukhosi alilala kwa rafiki yake wa kiume usiku wa kuamkia Jumapili, lakini vyanzo vingine vinadai kwamba binti huyo alishambuliwa na wazazi wake baada ya kufeli katika mtihani wa darasa la nane.
Gazeti la Nation halikuweza kupata uthibitishio huru juu ya madai hayo. Katika mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi (KCPE) aliofanya katika shule ya Ndalu, Abigael alipata alama 277 kati ya 500.
Michael Simiyu, ambaye ni jirani, Jumanne aliliambia gazeti la Nation kwamba mtu mmoja aliyetambuliwa kwa majina ya Meshack Barasa, alimpiga binti huyo hadi kufa aliporejea tu nyumbani.
"Yeye na mkewe walimfunga binti huyo na wakaanza kumwadhibu. Tukio hilo lilifanyika mchana," alisema Simiyu.
Social Plugin